Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua Duka la Huduma ya wateja mjini Shinyanga kwa lengo la kurahisha huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.


Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa duka hilo la huduma kwa wateja lililopo karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.

Awali akizungumza wakati wa kuzindua duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel nchini Sunil Colaso alisema wamezindua duka hilo ili kuongeza wigo wa soko mkoani Shinyanga na kuwasogezea huduma wananchi.

“Tunafuraha kubwa kufungua duka hili leo ambalo ni miongoni mwa maduka sita ambayo yanafunguliwa mkoani Shinyanga,hili ni duka la pili Mjini Shinyanga na tunatarajia kufungua maduka mengine ndani ya mwezi huu”,alieleza Colaso.

Aidha Colaso alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Shinyanga kufika katika duka hilo la huduma kwa wateja ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo kurudisha namba zilizopotea,kuuza laini,simu,kurekebisha namba za siri za Airtel Money na huduma nyinginezo.

Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema uwepo wa duka hilo utaongeza ajira kwa vijana na pia itarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za simu kwa wananchi ikiwemo huduma za pesa.

“Yanapofunguliwa maduka mengi inasaidia kupunguza umbali wa wananchi kufuata huduma,nawaomba wananchi kila mtu asajili simu yake kwa majina yake halisi ili kupunguza vitendo vya uhalifu",alisema Matiro.

“Nawaomba wananchi mtumie maduka haya kupata huduma mnazohitaji badala ya kutumia watu wa kati ambao baadhi yao siyo waaminifu,kumbukeni mawasiliano ni maendeleo,bila mawasiliano maendeleo yanakuwa ni shida,na sisi tunapoangalia vipaumbele vya maendeleo huwa tunaangalia pia kuna mawasiliano gani”,aliongeza Matiro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro katika duka la huduma kwa wateja wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo katika mtaa wa Buzuka karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga leo Jumanne Machi 14,2017.
Meneja wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja mjini Shinyanga. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma kwa wateja.Katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro na Afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga Mjini Simon Mashishanga wakimsikiliza mkurugenzi huyo wa Airtel.Picha zote na Kadama Malunde

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...