THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

AJALI YA GARI YATOKEA KIMARA SUKA JIJINI DAR ES SALAAM, WAMSHAMBULIA MWANDISHI ALIYEKUWA AKICHUKUA PICHA ZA TUKIO

Gari aina ya Mark II Grand yenye namba za usajili T145AMZ likiwa limeivaa daladala lenye namba za usajili T992DGZ lililokuwa limepaki kituoni KIMARA -SUKA jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wapo eneo la tukio ilionyesha dereva wa gari hilo dogo alikuwa amelewa na ndipo aliposhindwa kukamata breki na kujikuta uvunguni kwa daladala hilo.
Vijana wakijaribu kuiba katika gari ndogo iliyokuwa imepata ajali eneo la Kimara Suka jijini Dar es Salaam.
Vijana ambao walivamia gari ndogo na kuanza kuiba wakishangaa kuona kamera ya Kajunason Blog imetinga eneo hilo na ndipo walipoungana na mwenye gari kumfanyia fujo na kumpiga kwa kumshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna aliyekuwa eneo la tukio. 

Kwa msaada wa wasamalia wema waliweza kumnasua mwandishi huyo na kumshika kijana aliyekuwa mmiliki wa gari ndogo ambaye ndiye alitoa amri ya kumshambulia mwandishi wa habari.

 Kijana aliyemshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna amekamatwa na kufunguliwa jarada la KMR/RB/3987/2017 na mpaka sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Mbezi kwa Yusuph.