BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, leo imezindua bidhaa adimu itakayokuwezesha kuvuna riba hadi asilimia 16% kutokana na akiba maalum utakayojiwekea.

Katika hali ya kawaida kama tulivyozoea, amana za muda maalum zimekuwa kivutio kwa wateja wengi wa mabenki. Kwa kuanzia amana hii yenye riba kubwa ni nzuri kuliko kufungua akaunti ya akiba ya kawaida kwani unapata riba nzuri zaidi.

Faida nyingine ni  uhakika wa mapato ya riba na uwezo wa kuamua namna gani ya kuitumia, kukopa au kuweka akiba zaidi, utakavyopenda mwenyewe.

BancABC imechukuwa hatua kubwa zaidi kwa kutoa riba ya asilimia 16%, vilevile utapata riba hii bila ubabaishaji.

Akiongea jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wale wafanyabiashara wa kati. Mama Joyce Malai alisema hakuna tena nafasi nzuri ya kunufaika na huduma za benki kama hii iliyopo sasa.

 “Tunathamini mchango mzuri wa wateja wetu, kwa hiyo kama benki makini kupata ruzuku tunatoa huduma hii ya kipekee kama zawadi maalum”.

Hii haina tofauti ya kupata faida ya biashara hata kabla hujaianza!  Tunaamini tumeileta huduma hii kwa wakati muafaka, katika muda inayohitajika haswa.  Tuna hakika bidhaa hii mpya ya kibenki itawavutia wateja wengi  hasa wale walio makini”, alisema Joyce.
 Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati wa BancABC, akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa akaunti maalum ya JIONGEZE MARADUFU uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo. Kulia ni Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC.


 Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati,  na  Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC wakionyesha (bidhaa) Akaunti mpya na ya kipekee JIONGEZE MARADUFU iliyozinduliwa na BancABC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...