Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amepiga marufuku ukataji miti kwa ajili ya mbao na mkaa na kuagiza kila kaya kupanda miche 10 ya miti. Alitoa agizo hilo jana wakati akizindua kampeni ya upandaji miti kiwilaya iliyofanyika Kijiji cha Mwatuju Kata ya Shagihilu ambapo jumla ya miti 91,000 tayari imepandwa tangu msimu wamvua kupanda ndani ya kata 13 vijiji 28 imepandwa kwa ushirikiano na wadau wa mazingira.

Taraba alionya kuwa kaya isiposhiriki katika zoezi la upandaji miche ya miti mbalimbali itachukuliwa hatua kali ikiwemo kutakiwa kulipa faini. Alisema ukosefu wa mvua unatokana na kukosekana kwa miti na kuwa shughuli za kimaendeleo zinakwama ikiwemo wananchi kushindwa kulima mazao ya chakula na hata biashara.

“Hali hii inatokana na ukosefu wa miti, Kishapu hakuna mkaa wala mbao kwa hiyo ni marufuku kukata miti mpande miti mwezi wan ne tutakagua, atajayeshindwa atalipa faini shilingi elfu hamsini na tutazikusanya ili tuandae vitalu vya mwaka kesho,” alisisitiza.

Taraba ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya alishangazwa na madai ya baadhi ya wananchi kuwa miti inaleta wanyama aina ya fisi na kuwataka waache uoga.

Kwa upande mwingine alikemea tabia ya baadhi ya wafugaji kunyweshea mifugo kwenye vyanzo vya maji hali inayosababisha miti kushindwa kuota ambapo aliwataka wafuge kwa ustaarabu.  
Kiongozi huyo aliongeza kwa kusema kuwa miti ina faida nyingi ikiwemo vivuli wakati wa mikutano au sehemu za kupumzikia, matunda na kukuza uchumi katika wilaya hiyo. 

“Tumehangaika sana wenzetu wanapata mvua sisi hatupati mvua hiyo ni kutokana na kwamba hatuna nidhamu ya utunzaji miti hivyo ni lazima tupande miti ituletee hewa nzuri na mvua,” alisisitiza.
aliwashukuru wadau Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na utunzaji mazingira TCRS na mgodi wa Almasi wa Mwadui Williamson kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, George Kessy aliwataka wananchi waone umuhimu wa upandaji miti na kusema kuwa ndiyo uhai. Kessy ambaye pia ni Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika upandaji miti na ili isaidie katika kuleta mvua.

 Alisema kuwa mvua inaponyesha inasaidia wakulima katika kuotesha na kukuza kilimo cha mazao mbalimbali na hivyo kuleta chakula na kukuza uchumi wa wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba akipanda mti katika Kijiji cha Mwatuju Kata ya Shagihilu alipozindua kampeni ya upandaji miti kiwilaya jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akizungumza.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...