Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Filamu ya Kitanzania ya Kiumeni chini ya Muigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Ernest Napoleon itaonyeshwa kwa mara ya kwanza Jumatano hii katika ukumbi wa sinema wa Mlimani City Century Cinemax Jijini Dar es salaam.

Filamu hiyo ambayo imeandaliwa kwa kipindi cha miezi mitatu na kugharimu zaidi ya sh. milioni 50 imewakutanisha waigizaji kama Muhogo Mchungu, Irene Paul, Idris Sultan, Ernest Napoleon pamoja na waigizaji wengi wachanga ambao walionyesha uwezo mkubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Century Cinemax, Mlimani City Jijini Dar es salaam muda mchache baada ya waandishi kuonyeshwa filamu hiyo, Ernest Napoleon alisema filamu hiyo ni filamu ambayo itawafanya watanzania na wapenzi wa filamu nchini kupenda filamu zao kutokana ubora wa filamu hiyo.

“Kesho ni siku ambayo filamu yetu ya Kiumeni ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu itaonyeshwa kwa mara ya kwanza hapa Century Cinemax, Mlimani City. Kuanzia saa 12 jioni watu wataanza kupata picha za red carpet na saa mbili usiku filamu itaanza kuonyeshwa. Kwahiyo ni filamu ambayo tumeigizia uswazi kabisa, stori ni nzuri hata baadhi ya vijana ambao wameonekana tumewatoa huko huko mtaani na wengine hawakuwai hata kuigiza lakini wameonyesha uwezo mkubwa,” alisema Napoleon.

Aliongeza,”Filamu ni nzuri na ina ubora ndio maana hata hapa Century Cinemax tunaendelea kupewa nafasi, mara ya kwanza wakati tunazindua filamu ya Going Bongo tulipewa siku tatu za kuionyesha lakini baada ya kuona watu wanapenda wakatuongezea wiki na baadaye wiki mbili kwa maana ikaonyeshwa kwa wiki mbili. Filamu ya Kiumeni ilivyowafuata tu wakaniambia itaonyeshwa kwa wiki mbili. Kwa hiyo hiyo ni dalili nzuri kwa filamu zetu kwa sababu tulianza hawatuamini mpaka sasa wanatuamini,”

Pia alisema baada ya uzinduzi wa Tanzania ataenda kufanya uzinduzi nchini Kenya na baada ya hapo itaachiwa kwenye mfumo wa DVD ili iweze kupatikana nchini kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...