Naibu meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto ameviomba vikundi vya Jogging kuanza kujisajiri hili waweze kupata fursa za mikopo kutoka Halmashauri zao.
Kumbilamoto amesema hayo alipokuwa akizungumza mwishoni mwa wiki na Vikundi mbalimbali vya Jogging katika Bonanza lililoandaliwa na Mzimuni Joger na kushirikisha vikundi zaidi ya kumi .
"kila Halmashauri ina mapato ambayo inatakiwa kutoa kwa vijana ambayo ni asilimia 10 kwa vijana na vikundi vya kina mama hivyo vikundi vya Joging vinahusisha watu wote hao katika hivi vikundi vyetu" Amesema Kumbilamoto
Amesema ufike wakati wa Halmashauri zote zitenge pesa za vijana na kuacha ujanja ujanja wa kukwepa kulipia fedha hizi kwani kama wanashindwa waje kujifunza Ilala hili waweze kuwakwamua vijana na kinamama.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akizungumza wakati wa Bonanza la Klabu ya Mbio za pole za Mzimuni Joging
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Oamry Kumbilamoto akiongoza safu ya Wakimbiaji katika Bonanza la Mzimuni
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...