Na  Bashir  Yakub.

Matunzo  ya  mtoto  hasa  kwa  wazazi  waliotengana  ni  pamoja na  chakula,  makazi,  mavazi,  elimu,  pamoja  na  malezi  bora. Wazazi  wote  kwa  pamoja  yaani  baba  na  mama  wanao wajibu   kila  mmoja  kwa  nafasi  yake kuchangia  katika   matunzo  ya  mtoto.

Aidha  makala  haya  kupitia Sheria  ya  Mtoto ,Na. 21  ya  2009   yatajibu  ikiwa  suala  kutoa  matunzo  ya  mtoto  ni  la  milele  au  linao  muda  maalum.  Lakini  kabla ya  hayo  tutizame  nani  ana  mamlaka  ya kufungua  shauri  kudai  matunzo  ya  mtoto.

1. NANI  ANAWEZA  KUFUNGUA  SHAURI  LA  MATUNZO.

Wengi  wetu  twajua  kuwa  ni mama  wa  mtoto  pekee  ndiye  anayeweza kufungua  shauri  la  mtoto  kupatiwa  matunzo.  Dhana  hii  si  kweli.
Kifungu  cha  42( 1 )   cha  Sheria  ya  Mtoto  kinawataja  wafuatao  kuwa  na  mamlaka  ya  kuomba  mtoto apatiwe  matunzo :

( a ) Mzazi  wa mtoto.  Kifungu  hakikutaja  mama  wa mtoto  bali  mzazi  wa  mtoto. Kwahiyo  hata  baba  anaweza  kufungua  shauri  akimtaka  mama  kutoa  matunzo  ya  mtoto.  Mama  kumtelekeza  mwanae   nako ni kumnyima  mtoto  matunzo  .
Wako    mama  wanakimbia  nyumba  zao  na  kuwaacha  watoto. Unaweza  kutumia  kifungu  hiki  kumtaka  mama amchukue  mwanae  na  akae  nae  ikiwa  ni  sehemu  ya  matunzo.

( b ) Mlezi  wa  mtoto  naye  amepewa  mamlaka  ya  kufungua  shauri  kuomba  matunzo  ya  mtoto.  Wako  watu  wako  mjini  lakini  wamewaacha  watoto  vijijni  wakilelewa  na   ndugu au  rafiki.

Lakini  pia  yapo  mazingira  ambapo  kwa  amri  ya  mahakama    imeamriwa  mtoto  asikae  na  wazazi  bali  akae  na  mlezi  kutokana  na sababu  mbalimbali. Au  kwasababu  nyingine  yoyote mtoto  anakaa  na  mlezi .

Basi  ni  katika  hali  hiyo  mlezi  huyo  anayo  mamlaka  ya  kuomba  au  kufungua  shauri  akishinikiza  mzazi/wazazi  kutoa  matunzo  ya  mtoto.

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...