THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA AZAM MEDIA

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyesimama) akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakati  Kamati  hiyo  ilipotembelea Azam Media jana Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Azam Media Bw.Tido Muhando.
 Mkurugenzi wa Azam Media Bw. Tido Muhando (aliyesimama) akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) utendaji kazi wa Chombo hicho wakati  Kamati  hiyo  ilipotembelea Azam Media jana Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Faustine Ndugulile akizungumza  jambo  kwa Kamati hiyo na uongozi wa Azam Media wakati Kamati ilipotembelea chombo hicho jana Jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Mkurugenzi wa Azam Media Bw. Tido Muhando(hayupo pichani ) wakati Kamati ilipotembelea chombo hicho jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wa kwanza kushoto akizungumza na wasikilizaji wa Uhai Radio wakati  Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ilipotembelea studio hizo jana Jijini Dar es Salaam.