Na Fredy Mgunda,Mafinga

Kikosi cha jeshi la kujenga Taifa 841kj mafinga, kimeanzisha kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha jeshi hilo linajilisha na kupata mahitaji mengine kupitia uzalishaji mali.

Akizungumza kaimu kamanda wa kikosi cha 841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 / 1967 kikiwa na lengo la kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa na serikali ya viwanda kwa kuanza kujenga kiwanda cha nafaka na mifugo ambacho kitatoa ajira wa watu wengi na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja na kuimalisha ulinzi kutokana na majukumu waliyonayo.

Nkya alisema kuwa kikosi cha 841kj kj mafinga kimeamua kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa kinaendeshwa kibiashara ili kukuza ajira na pato la taifa.

“Hapa kikosini tunalima na kufuga mifugo ya aina mbalimbali kwa wingi na kwa kiwango kinachotakiwa kukidhi soko ili kuonyesha kuwa kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kinakuwa mfano wa kuigwa na kukidhi haja ya kuanzishwa kwa kikosi hicho”.alisema Nkya
Mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 pamoja na kuzindua jarida maalum la kikosi hicho akiwa amelishika linaitwa Uhodari. 
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 841kj wakionyesha ukakamavu wake kwa kushindana kuvuta kamba ikiwa na lengo la kuburudisha wakati wa sherehe za miaka 50 ya kikosi cha 841kj
Baadhi ya vijana waliopo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi maarufu kama operation Magufuli kujitolea katika kikosi cha 841kj mafinga nao walikuwa miongoni mwa waliosherekea miaka 50 ya kikosi hicho.
Hili ndio jengo linalojengwa kwa ajili ya kiwanda cha Kukoboa na kusaga nafaka za kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...