MAREHEMU JANUARY CLAUDIO KISANKO

Leo tarehe 21-Machi-2017 Baba yetu mpendwa ametimiza mwaka mmoja tangu alipoitwa na Mwenyezi Mungu. Tunaamini yupo nasi kiroho na daima tunamshukuru Mungu kwa muda wote aliokuwa nasi.

Misa ya kumbukumbu itafanyika siku ya Jumamosi, Machi 25, 2017 saa mbili kamili asubuhi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Bonaventura Kinyerezi mwisho jijini Dar es salam. Familia inawakaribisha wote siku hiyo kanisani na baadae kwenye chai nyumbani kwa marehemu Kinyerezi mwisho.
Tunamwomba Mungu azidi kuipumzisha Roho yake mahali pema peponi. AMINA

Raha ya Milele umpe ee Bwana, 
na Mwanga wa Milele umwangazie. 
Apumzike kwa Amani. Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...