NA  BASHIR  YAKUB -


Je  nani  anawajibu  wa  kumtunza  mwenzake  kati  ya  wanandoa.  Je  ni  mme,  je  ni  mke   au  ni  wote .  Sheria  inasemaje  kuhusu  hili. Kwa  kuanza  tu  ni  kuwa  suala  matunzo  kwa  wanandoa  ni  la  kisheria. Matunzo  sio  hisani,zawadi  au  upendeleo  maalum  bali  ni  wajibu  uliozaliwa  na  sheria.

Sheria  ya  Ndoa  iliyofanyiwa  marekebisho  mwaka  2010 ,  sura  ya  29 imeweka  bayana  habari  nzima  ya  matunzo  baina  ya  wanandoa. Niseme  mapema  tu  kuwa wapo  wanaojua  kuwa mme  peke  yake ndiye  mwenye   wajibu  wa  kutoa  matunzo  kwa  mke. Tutaona  hili  likoje .  

Kabla  ya  hayo   ni  vema  tukaona  matunzo  yanajumuisha  nini  na  nini  kwa  mujibu  wa  sheria  hii.

1.MATUNZO  NI  YAPI.

Kifungu cha  63( a ) cha  sheria  ya  ndoa  kinataja  vitu  ambavyo  kisheria  ndivyo  vitakavyoitwa  matunzo  kwa  mwanandoa. Kifungu  kinataja makazi(accommodation),  mavazi, na  chakula.  Haya  ndiyo  ya  msingi  ambayo   mwenye  wajibu  wa  kuyatoa  atatakiwa  kutoa.

2.  MKE  KUTOA  MATUNZO  KWA  MME.        

Ni   vema  kujua  kuwa  suala  la matunzo  linawahusu  wanandoa  wote  yaani  mke   pamoja  na  mme.  Kila mmoja  anao  wajibu  kwa  mwenzake  katika  kutoa  matunzo. Isipokuwa  wajibu  huu  umetofautiana   kati  ya  hawa  wawili .  Mke  ana  wajibu  wenye  mipaka  katika  kutoa  matunzo   halikadhalika  mme.

Kifungu  cha  63( b )  cha  sheria  ya  ndoa  kinasema  kuwa  mwanamke  ambaye  ana  uwezo  anawajibu  wa  kutoa  matunzo  kwa  mme wake  ambaye  hajiwezi, ambaye  ana  ugonjwa  wa  kimwili  au  kiakili  ambao  haumuwezeshi  kufanya  kazi  ya  kumuingizia  kipato.

Kifungu  kiko  wazi  kuwa  wajibu   wa  mwanamke  kumhudumia  mwanaume  ni  pale  tu  mwanaume  huyo  anapokuwa  mlemavu  au  mgonjwa  wa  akili  au  mwili.  Lakini  pia  ugonjwa  huo  au  ulemavu  huo   uwe  ni  wa  kiwango  cha  kutomwezesha  kufanya  kazi. Ikiwa  ugonjwa  au  ulemavu  ni wa  kiwango  cha  kumwezesha  kufanya  kazi  atakuwa  nje  ya  muktadha  wa  kifungu  hiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...