THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI ATAHADHARISHA WANANCHI UPATIKANAJI WA MAFUTA ISIWE SABABU YA KUBWETEKA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametahadharisha Wananchi kwamba itakapofikia hatua ya kupatikana kwa rasilmali ya Mafuta na Gesi Asilia Visiwani Zanzibar isijekuwa chanzo cha sababu ya Wananchi kubweteka na mradi huo kwa kuacha shughuli zao za Kiuchumi ambazo huwapatia riziki zao za kila siku.

Alisema Rasilmali hiyo endapo itapatikana kufuatia utafiti unaoanza kufanywa hivi sasa itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto nyingi zinazoikabili Serikali Kuu pamoja na Wananchi kwa ujumla.Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa Ndege itakayofanya Utafiti na hatimae uchimbaji wa Rasilmali ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume nje kidogo ya Kusini ya Mji wa Zanzibar.

Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika yaliyoanza kuzalisha miradi hiyo kwa matumaini makubwa ya kuimarisha Uchumi wao lakini hivi sasa zimekuwa na changamoto zaidi za Kiuchumi hali ambayo Zanzibar na Wananchi wake wanapaswa kuwa makini na
kujifunza matukio hayo.

Hata hivyo Balozi Seif alisema safari ya Zanzibar kuelekea kwenye uchumi Mkuu imeanza mara baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitisha Mswaada wa kuanzisha sheria inayoiruhusu Zanzibar kutafuta na kuchimba mafuta yake yenyewe na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mainduzi kusaini Sheria hiyo.

Alisema busara za Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete za kusimamia utaratibu wa kupelekwa mswada Bungeni zimepelekea suala la mafuta na Gesi Asilia hivi sasa kutoka katika mambo ya Muungano.

Msimamizi wa Kampuni itakayofanya Utafiti waUtafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Bell Geospace  Inteprises Limited Bwana Stephane Kunar kushoto akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi Kulia nanma ndege Maalum itakavyofanya utafiti huo katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar. Kati kati ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira  mhg. Salama Aboud Talib, wa nyuma yake ni Katibu Mkuu wake Nd. Ali Khalil Mirza na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mhmoud.

  Balozi Seif akiangalia baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyochunguza maeneo yenye daliliza uwepo wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
 Balozi Seif  akijaribu kugusa vifaa vitakavyotumika katika kazi kufanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia sehemu zenye dalili ya uwepo wa Mafuta na Gesi Visiwani Zanzibar.
 Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA