Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamagana wameibuka washindi kwenye mashindano elimishi kwa klabu za mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani dhidi ya wakubwa zao kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma, zote za Jijini Mwanza.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) ya Jijini Mwanza, yalijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo maigizo, ngonjera pamoja na mashairi yenye jumbe za kuainisha aina za ukatili wanaokumbana nao watoto wafanyakazi wa majumbani ikiwemo vipigo, utumikishwaji na fursa ya kukosa elimu, na kuiasa jamii kuachana na vitendo hivyo.

"Ukiona mtoto anatendewa ukatili wa aina yoyote, paza sauti (toa taarifa) sehemu mbalimbali ikiwemo WoteSawa, polisi kupitia kitengo cha dawati la jinsia, kwa Mwenyekiti wa Mtaa ama Mtendaji wa Kata". Amesisitiza mgeni rasmi, Wambura.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya WoteSawa, Angel Benedicto, amebainisha kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo kutumikishwa kwa kuajiriwa ili kutembeza bidhaa mtaani kwa ujira mdogo, kunyimwa fursa ya kusoma pamoja na vipigo kutoka kwa baadhi ya waajiri hivyo taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu katika jamii ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.

"Lengo ni kupunguza ukatili wa watoto majumbani, kulinda haki za watoto, kuibua vipaji ikiwemo uchoraji na uigizaji ili kuvitumia katika kufikisha elimu ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto". Imefafanua sehemu ya risala ya klabu za wanafunzi mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya msingi Nyamagana na Nyakurunduma sekondari, iliyosomwa na Neema Christopher. 
Shule ya msingi Nyamagana wakifurahia ushindi wao ambapo igizo wamepata asilimia 93 dhidi ya 92 za Nyamagana sekondari, Shairi Nyamagana wamepata asilimia 74 dhidi ya 85 za Nyakurunduma huku Ngonjera Nyamagana wakipata asilimia 91 dhidi ya 77 za Nyakurunduma. Ushindi wa jumla, shule ya Msingi Nyamagana wamepata asilimia 86 dhidi ya 85 za Nyakurunduma sekondari.
Mabalozi kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma wakipokea kombe baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo
Pia mabalozi wote wamepatiwa vyeti kwa kujitoa kuwa mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...