Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii Agnes Gerald Waya maarufu kama Deal ama Masogange (28) bado haujakamilika.

Kesi hiyo imekuja leo kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashauru lakini wakati ikiahirishwa mshtakiwa Masogange alikuwa hajawasili mahakamani hapo. "mheshimiwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa hayupo" amesena wakili wa Serikali, Adolf Mkini

Kabla mahakama haijasema kitu,  wakili wa Masogange, Nictogen Itege aliwasilisha udhuru mahakamani hapo juu ya mteja wake kutokuwepo.

"Mheshimiwa hakimu, naomba udhuru, mshtakiwa yuko njiani anakuja mahakamani lakini amekwama kwenye Foleni Jangwani, tumekuja kwa njia tofauti" amesema Wakili Itege.

Hata hivyo, Hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa kuheshimu masharti ya mahakama na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 20, mwaka huu.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam. Anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam  alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017  alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Masogange yupo nje kwa dhamana ya kuwa na  wadhamini wawili wanaoaminika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kumshitaki muathirika wa dawa za kulevya mahakamani ni kutokuelewa maana hata kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya ambao ni wataalamu wanaojua hili tatizo vizuri hawawezi kamwe wakamshitaki mahakamani muathirika wa madawa ya kulevya.
    Wanaoshitakiwa mahakamani na kuadhibiwa ni wauzaji na wasambazaji.
    Wanachotakiwa ni kuuliza tu kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya kwanini hawawashitaki mateja mahakamani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...