MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi CUF Alhaj Mussa Mbaruku amemuomba Waziri wa Viwanda na biashara Charles Mwijage kuingilia kati ucheleweshawajiwa wa cheti cha ubora wa viwango unaotolewa na shirika hilo la TBS na kusababisha zaidi ya watumishi 300 kupoteza ajira baada ya  kiwanda hicho kufungwa.


Ameyazungumza hayo jana baada ya siku kadhaa kutolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa shirika hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza ajira kwa zaidi ya watumishi 300 kutokana na agizo lao la kusitiza uzalishaji katika kiwanda hicho kwa madai ya kukosa ubora unaotakiwa.



Alionyesha masikitiko yake hayo juu ya hataua iliyochukuliwa na shirika hilo la Ubora wa viwango Tanzania (TBS) ya kukifungia kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro kilichopo Jijini Tanga kwa kudaiwahawajafikia ubora unatakiwa katika bidhaa hiyo bila ya kuangalia athari za mwekezaji huyo na ajira zilizopotea kiwandani hapo.

Aidha alisema ni jambo la kushangaza kwa viongozi wa mamlaka hiyo husika(TBS)ambapo kwa namna moja au nyingine wanaonekana wanaikwamisha Serikali katika mpango wake wa kukua katika uchumi wa viwanda ambavyo vinaweza kuwa mkombozi wa ajira hapa nchini.


“Serikali inapambana na uchumi wa viwanda vitakavyoweza kusaidia ajira kwa vijana wetu sasa kinachotokea katika kiwanda hiki kunaonekana kuna watu wachache wanataka kumkwamisha muwekezaji huyu,hivi wizara husika iko wapi?nini hatma ya mwekezaji huyu na kufanya hivi hatuoni kama tunawafukuza hawa wawekezaji?”Alihoji Alhaj Mbaruku.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusiana na suala hilo.
 Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutotoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitisha  uzalishaji
Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha
Kilimanjaro ,Vivek Pandey  kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika wa kiwanda hicho  na hivyo kusitisha uzalishaji kulia ni Msimamizi wa Kiwanda hicho,Paskal Dimelo
Msimamizi wa Kiwanda cha kuzalishaji Saruji Mkoani
Tanga cha Kilimanjaro, Paskal Dimelo akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitiza uzalishaji wake kushoto ni Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...