MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameahidi kuchangia mifuko 100 ya Saruji pamoja na Mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Maweni iliyopo Kata ya Mjimwema wilayani Kigamboni. Shule hiyo ambayo inaupungufu mkubwa wa madarasa pamoja na uzio wa shule , inajumla ya wanafunzi 1300 ikiwemo na wale wenye ulemavu.

Akizungumza katika hafla hiyo  ya chagizo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, Meya Isaya alisema kwamba hatua hiyo ni kwa ajili ya kuzisaidia shule ambazo zinaupugufu wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi wasome katika mazingira salama.

Alisema kwamba wakati alipokuwa akiwania nafasi ya Udiwani Kwenye kata yake ya Vijibweni , na kisha kupata nafasi ya kuwa Meya wa jiji, moja ya vipaumbele vyake ilikuwa ni kuzisaidia shule ili  kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukaa. 

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema, Selestine Maufi pamoja na mambo mengine alimpongeza Meya Isaya kwa kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa kwa ajili ya kujenga madarasa katika shule hiyo. Hata hivyo Diwani huyo aliahidi kuchangia matofali 500 ,madawati 60 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa .

Hata hivyo awali akisoma lisara kwa mgeni rasmi iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo, Mwalimu Selemani alisema kwamba shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba kadhaa vya madarasa ambapo vilivyopo havikidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo.

Alifafanua kwamba kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa wananfunzi wenye ulemavu wamelazimika kusomea kwenye chumba cha darasa kimoja jambo ambalo linawapa shida walimu kwenye ufundishaji.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko na Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche.PICHA NA ELISA SHUNDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...