Katika mpango wa kuboresha makazi yaliyojengwa kiholela, Kimara imekuwa mojawapo wa maeneo yanayoendelea na zoezi la Urasimishaji. Kwa sasa hatua iliyofikiwa ni ya uwekaji wa barabara za mitaa.
Halmashauri nyingine 6 zilizopangwa kutekeleza mradi huu ni; Manispaa za Musoma, Kigoma-Ujiji, Tabora, Singida, Sumbawanga na Lindi ambapo viwanja 3000 vitapimwa katika kila Halmashauri.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi inatekeleza mradi wa kurasimisha maeneo yaliyojengwa kiholela katika Jiji la Dar es Salaam katika kata ya Kimara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Ubungo. Jumla ya viwanja 6,000 vinatarajiwa kupimwa na kumilikishwa. Katika mitaa ya Makongo juu, na Chasimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo jumla ya viwanja 6585 vitapimwa.
Urasimishaji utaongeza huduma za jamii na miundombinu katika makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa hati za kumiliki ardhi kwa muda mrefu. Mpango huu unatekelezwa kwa kushirikisha wananchi na viongozi wa maeneo husika.
Katika mpango huu, Wananchi wanawajibika kuonyesha mipaka ya miliki zao pamoja na kuchangia ardhi kwa ajili ya barabara. Aidha kila mwananchi anawajibika kutoa taarifa kwa usahihi ili kurahisisha umilikishaji. Urasimishaji unatekelezwa kulingana na sheria ya Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999 fungu la 56-60
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawasihi Wananchi kushirikiana vyema katika zoezi hili kote nchini ili kuepuka  Makazi holela kwa Maendeleo ya Taifa.
Vile vile, Wizara itaendelea kushirikiana na Halmashauri nchini kuandaa mipango ya zoezi la Uramishaji. Baada ya Urasimishaji; miji inatarajiwa kuendelezwa kwa kulingana na mapendekezo ya mipango kabambe.
 Mjumbe katika kamati ya Mipango Miji – Chasimba; Bi Hawa Haruna Kimaro akitoa maelezo kwa Wananchi kuhusu zoezi la upimaji linavyoendelea  Chasimba.
 Zoezi la Urasimishaji linavyoendelea Kimara, ambapo zoezi hilo lipo kwenye hatua ya uwekwaji wa barabara za mitaa.
 Afisa Mipango Miji, akiwa katika zoezi la upimaji Chasimba.
 Dhana ya ushirikishwaji wa Wananchi inavyotekelezwa katika zoezi la Urasimishaji; Wananchi wakieleweshwa  na wapima  jinsi upimaji unavyofanyika katika eneo la Chasimba
Wananchi wakishuhudia uwekaji wa Barabara katika mitaa yao – Kimara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...