Makete: Lori lenye namba za usajili T 721 BVV lililokuwa limebeba mawe likiwa limepinduka katika kijiji cha Masisiwe na kusababisha majeruhi na kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa katika lori hilo

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa lori hilo lilipoteza muelekeo ghafla kisha likaanza kupinduka kwa kubiringika mara kadhaa umbali unaokadiriwa kuwa zaidi ya mita 80 kutoka barabarani

Ajali hiyo inadaiwa kutokea kati ya saa nane na saa tisa alasiri hii leo



Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema Lori hilo lilikuwa limetoka kubeba mawe kwa ajili ya kujenga daraja katika kata ya Ipepo na likiwa njiani kueleka eneo la ujenzi lilipopoteza muwelekeo na kupinduka kisha kuporomokea bondeni

Jeshi la polisi Makete lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi

Tutawaletea taarifa kamili ya tukio hilo pindi mamlaka husika zitakapatia.habari/picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog


Lori hilo linavyoonekana baada ya kupinduka.
Polisi wakipima jinsi ajali hiyo ilivyotokea.


Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...