Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

MAUAJI kwa viongozi wa vijiji na vitongoji mkoani Pwani hususan wilayani Rufiji vimeendelea kukua ambapo mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo wilayani humo Hemed Njiwa (45) ameuawa kwa kupigwa risasi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi ambae anahamishiwa mkoa wa Simiyu alisema Marehemu aliuawa na watu wasiojulikana  wakati akiwa nyumbani kwake.

Tukio hilo linadaiwa kutokea  usiku wa kuamkia machi 13 ,eneo la Kifuru kata na tarafa ya Ikwiriri wilayani hapo.
“Marehemu alipigwa risasi kifuani akiwa nyumbani kwa mke wake mdogo Maimuna Abdallah (36) na alikutwa na jeraha la risasi kwenye mkono wake wa kushoto”

Kamanda Mushongi, alieleza kwamba mtu ama watu waliohusika na tukio hilo baada ya kumwua alikimbia kusikojulikana kwa kutumia pikipiki aina ya boxer ambayo haikuwa na namba za usajili.

Alisema hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa na jeshi la polisi linaendelea na msako mkali ili kuweza kubaini watu waliohusika na tukio hilo.

Kamanda huyo aliwataka wananchi kuwafichua watu wanaohusika na matukio ya kuua viongozi wa vijiji na vitongoji kwani hilo linaweka idadi ya matukio zaidi ya matatu yaliyohusisha viongozi hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...