THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NGOMA, TAMBWE WAENDELEA KUUGUZA MAJERAHA WAKATI YANGA IKIJIFUA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mechi ya marudiano ya michuano ya  klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zanaco utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa Jumamosi Machi 18, itachezwa Nchini Zambia ambapo katika mchezo wa awali timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa kikosi kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo wa marudiano utakaofanyika nchini Zambia huku washambuliaji wawili wa kimataifa wakiwa hawajajiunga na wenzao.

Saleh amesema, Amisi Tambwe na Donald Ngoma bado wapo katika uangalizi wa daktari na hawajajiunga na wenzao katika mazoezi kuelekea mechi ya marudiano.

"Kwa sasa tunaendelea na mazoezi hapa Uwanja wa Taifa, Tambwe na Ngoma wakiwa hawajajiunga na wenzao kwani bado wapo chini ya uangalizi wa daktari, wachezaji wengine wote wapo fiti wakiendelea kujifua" amesema Saleh.

Kesho kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina anatarajia kutaja kikosi kitakachoondoka siku ya Alhamis kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya marudiano na Zanaco na Yanga inahitajika kupata ushindi wa goli 1-0 ili iweze kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya klabu Bingwa Afrika.