Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao (kulia)  akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas (kushoto) akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao.
 Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akitoa mada juu ya hali halisi ya uhuishaji wa Taarifa za Serikali kwenye Tovuti Kuu ya Serikali na Taasisi za Serikali katika Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano  Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. 
 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (Maelezo) Bi. Zamaradi Kawawa akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kutumia tovuti za ofisi na tovuti kuu ya Serikali kwa kuweka taarifa mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa zinazotolewa na taasisi hizo ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu huduma hizo kirahisi.

Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akitoa semina juu ya matumizi na umuhimu wa tovuti za Serikali katika kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea Mkoani humo.

Dkt. Bakari amesema dhana ya Serikali Mtandao ni  kuhuisha matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi hivyo ni muhimu kwa kila taasisi kuwa na tovuti zenye taarifa za uhakika na zinazoendana na wakati ili  kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

“Wakala kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tumetengeneza mfumo unaotumia muda mfupi kwa taasisi za Serikali kutengeneza tovuti zao ili ifikapo Juni mwaka huu taasisi zote ziwe na tovuti zao zitakazowarahisisha wananchi kufahamu huduma kirahisi,”alisema Dkt.Bakari.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...