Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani ambao utawezesha vijiji mbalimbali katika mkoa huo kupata huduma ya Umeme.

Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa.

Uzinduzi wa mradi huo ulienda sambamba na utambulishaji wa Mkandarasi atakayetekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo ambaye ni kampuni ya Steg International Services.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga alieleza kuwa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu unahusisha vipengele Mradi vitatu vya utekelezaji.

Alisema kuwa kipengele cha kwanza cha utekelezaji kitahusisha kufikisha umeme kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa kabisa na miundombinu ya umeme wa gridi na kipengele cha Pili kitahusika na kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...