Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


KAMPUNI ya Quality Group imedhamiria kuendelea kujikita zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo za madini, kilimo cha sukari na kuanzisha kwa kiwanda na  usambazaji wa  matrekta nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni hayo Nicholaus Raphl   Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kampuni ya Quality toka ianzishwe nchini imeweza kuajiri wafanyakazi zaidi ya laki sita (667,300) na imejikita zaidi katika kuwaajiri wazawa.

Quality Group katika kukuza sekta ya viwanda nchini imeingia mkataba na kampuni ya Solanika International Tractors Limited na mradi huo utaanzia mkoa wa Morogoro ambapo takribani matreka 1000 yataanzia kule na watanzania takribani 1200 watapata ajira na mradi huu utakamilika 2018.

Uanzishwaji wa mradi huo utawasaidia watanzania kupata matreka yatakayokuwa na ubora mzuri na yatakuwa ya bei nafuu na kila mkulima anaweza kuwa nalo kwani yatatengenezwa hapa hapa nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Solanika.

Pia, Raphl amesema Quality wamedhamiria kuwekeza zaidi katika sekta ya afya kwa kujenga vituo 4,000 vya afya sehemu mbalimbali nchini na itamuwezesha kila mwananchi kupata tiba sahihi na itakayokidhi umuhimu wa mgonjwa na tayari kampuni kutoka nchini Urusi wameshaingia nao makubaliano ya kusambaza dawa kwenye vituo hivyo.

Mbali na hayo, Quality wameweza kujikita katika kukuza elimu ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali wa uvuvi kwa wananchi wanaoishi kando ya Ziwa Victoria na kuwapatia vifaa vinavyostahili kwa kutumika kwenye uvuvi.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Quality Group Nicholaus Ralph akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya kimaendeleo itakayofanywa na kampuni hiyo.
Baadhi ya Wanabari wakifuatilia mkutano huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...