Raisi wa Uganda, Yoweri Kaguta Museven amelaani mauaji ya Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda ambaye pia alikuwa ni Naibu Mkuu wa Jeshi hilo, Andrew Kaweesi na walinzi wake wawili ambao walishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala, Nchini Uganda jana. 

Bado haijajulikana sababu hasa ya kutekelezwa mauaji hayo ingawa serikali imeagiza kufungwa kwa kamera za usalama katika miji mikubwa yote nchini humo wakati huu uchunguzi ukifanywa.

Katika kipindi cha miaka saba iliyopita takribani matukio ya mauaji 12 yametekelezwa na washambuliaji waliokuwa wakiendesha pikipiki maarufu kwa jina la boda boda ambao walitoroka eneo la tukio na kutopatikana licha ya jitihada za polisi kuendelea kufanyika kuwatafuta.

Kwa mujibu wa Luteni Jenerali, Henry Tumukunde, mara nyingi vitendo hivi hufanyika kwa umakini kujiamini na ujasiri huhakikisha wameua kabisa kabla ya wauaji kutokomea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...