THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RC MAKALLA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI NA MILA KUWAEPUSHA WANANCHI NA IMANI ZA KISHIRIKINA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala  ameitisha kikao na viongozi Dini na mila kuwaomba msaada wa kukemea vitendo vya kishirikina katika mkoa huo. Makala amesema hayo katika kikao chake na Viongozi hao pamoja na wenyeviti wa mitaa na vijiji katika mkoa wa Mbeya.

"matukio ya watu kufukua maiti au kutozika kwa imani ya kuwafuafua  hayapaswi kuachwa yaendelee , Biblia na Qurhan imeandikwa kuna kufufuliwa, kuna kiama ,kuna pepo ni baada ya kufa nawaomba  mnisaidie   kutoa Elimu na mafundisho yenye kuondosha matukio hayo" Amesema Makalla.

 Makalla awaomba pia kusaidia serikali katika mapambano ya Dawa ya Kulevya kwa kutoa Elimu na hamasa ya kuelimisha madhara ya dawa ya kulevya.

Amesema Mbeya itangazwe kwa sifa nzuri kama Mkoa unaotegemewa kwa uzalishali wa Chakula, Mkoa wa tatu kitaifa kuchangia pato la Taifa na ni Mkoa unapiga hatua kubwa kimaendeleo.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na viongozi wa Dini, viongozi wa mila, na mitaa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa leo jijini Mbeya.
 Baadhi ya viongozi wa dini na serikali za mitaa na mila wakiwa katika ukumbi wa mkapa kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla.
Mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla watatu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya mbeya mh.William Ntinika (kushoto) Pamoja na viongozi wa Dini mkoa wa Mbeya.