Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema jiji la Dar es Salaam linatakiwa kubadilika  katika kufikia viwango vya majiji ya kimataifa. Makonda ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja, amesema  barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.

Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.

"Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sita haijapita" amesema Makonda .

Amesema barabara hiyo imejengwa na kampuni ya kizalendo ya Grant Tech Company ya jijini Dar es Salaam na maombi ya barabara ni miezi miwili iliyopita lakini imekamilika kwa muda mwafaka .

Makonda amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile. Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza adha za usafiri kwa  wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta hitilafu hata kwa vyombo vyao vya usafiri.

Makonda amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni  ndoto ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda  inaendelea kutimia.

Mkandarasi huyo (Grant tech), Masito Mwasingo amesema kuwa wamefanya ujenzi kwa muda mwafaka kutokana umuhimu na kuunga kuunga mkono utendeji kazi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva na watendaji wakitembelea barabara Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa wa akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza katika uzinduzi wa kukabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva  wakikata utepe kuashilia kukabidhiwa barabara ya Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Baarbara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Very impressive. I wish barabara kama hizi zijengwe zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...