Na
Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu
ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imepangwa
Kundi B katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya
umri wa miaka 17, zitakazofanyika nchini Gabon kuanzia Mei 14 hadi 28, mwaka
huu.
Serengeti
walifuzu kuingia katika fainali hizo baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya Congo
Brazaville kushindwa kumpeleka mchezaji wao aliyechezeshwa kwenye kikosi cha
vijana lakini akisadikiwa kuwa ni mkubwa kiumri tofauti na kanuni za mashindano
hayo.
Congo
Brazaville walishindwa kumuwasilisha kwa vipimo zaidi ya mara tatu
walipohitajiwa na CAF na hivyo CAF kuamua kuwaondoa kwenye nafasi hiyo na
kuchukuliwa na Tanzania..
Kundi
B, Serengeti Boys wamepangwa na Angola, Niger na Mali ambapo kwa sasa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limewafungia baada ya Serikali ya
nchi hiyo kuingilia masuala ya soka na kuwafukuza viongozi wa Shirikisho
la Soka la nchi hiyo (FEMAFOOT).
Kundi
A lina timu za wenyeji Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana na ikumbukwe timu mbili
za juu kila kundi zitafuzu moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia za U-17 nchini
India baadaye mwaka huu.
Awali fainali hizo zilitakuwa
kufanyika nchini Madagascar lakini Gabon aliyekuwa rais wa Shirikisho la
Soka Afrika (CAF) Issa Hayatou wa Cameroon alisema nchi hiyo
haikukidhi vigezo vya kuandaa mashindano hayo.
Kikosi
cha timu ya Tifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...