Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Kituo cha msaada wa kisheria kwa Wanawake (WLAC) kimeishauri serikali kufanyia marekebisho ya sera na sheria mbalimbali kandamizi zinazochangia vitendo vya ukandamizaji, unyanyasaji na ukatili kwa wanawake nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika semina ya vijana wa Wilaya ya Ubungo ya kuwajengea uwezo, utungaji, uchambuzi na utekelezaji wa sera mbalimbali, mwanasheria wa WLAC Karilo Mlembe Karilo amesema sheria hizo zinachangia kwa kiwango kikubwa vitendo vya ukatili kwa wanawake.

Amesema, baadhi ya sheria ambazo zinasababisha vitendo vya ukatili ni sheria ya mirathi ambayo haimpi fursa mwanamke kurithi Mali pindi anapofiwa na mumewake hata kama alishiriki katika upatikanaji wa Mali hizo isipokuwa watoto wake.

Aliitaja sheria nyingine kuwa ni sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kutolewa kwa idhini ya wazazi au Mahakama.

Mbali na sheria kandamizi pia alisema zipo baadhi ya Sera zinazokandamiza upatikanaji wa haki Kwa wanawake kupata ajira na kwamba kwa ujumla wake ni vem serikali ikafanya utaratibu wa kuboresha sheria za Sera zote zinazochangia kumkandamiza mwanamke katika upatikanaji wa haki zake.

Naye muwezeshaji wa semina hiyo, Israel Ilunde, amesema Sera na sheria zimepitwa na wakati kwa sababu zilitungwa kuendana na mahitaji ya wakati huo, hivyo kunahitajika maboresho ya sheria zitakazoendana na mahitaji ya sasa.

"Na ndio maana leo tunawafundisha hawa vijana namna ya kufanya uchambuzi wa sheria na sera mbali mbali kandamizi ili kuhamasisha jamii namna ya kushiriki katika mijadala na kujenga hoja zinazolenga upatikanaji wa were na sheria bora", amesema Ilunde.
Muwezeshaji wa semina ya vijana ya utunngwaji, uchambuzi na utekelezaji wa sheria, Israel Ilunde, akiendesha semina hiyo kwa Vijana wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa WALC, Karilo Mlembe akiongea na vijana wa Wilaya ya Ubungo wakati wa semina ya utungwaji na uchambuzi wa sera na sheria, jijini Dar es Salaam
Vijana wa Wilaya ya Ubungo wakifuatilia mafunzo ya semina ya utungwaji, uchambuzi na utekelezaji wa sheria, iliyoandaliwa na WLAC jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...