Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zitakazofaidika na mpango wa kuwakinga wanafunzi wa shule za msingi kupata ajali za barabarani ulioanzishwa na shirika la kimataifa la Amend kwa msaada mkubwa wa taasisi ya FIA Foundation na Puma Energy Foundation. 


Mpango huo ulizinduliwa juzi kwenye shule ya msingi mpakani iliyopo Manzese Tip Top ambao lengo kubwa ni kujenga miundombinu itakyosaidia wanafunzi kuepuka ajali za barabarani waendapo, wakati wa kuvuka na kurejea kutoka shuleni.

Nchi nyingine ni Benin, Botswana, Ivory Coaste, Ghana, Malawi, Mozambique, Namibia, Senegal na Zambia.

Mkurugenzi wa mpango huo kutoka shirika la Amend, Ayikai Poswayo kutoka Ghana alisema kuwa takwimu si nzuri kwa Tanzania kuhusiana na ajali za barabarani ambapo inakadiliwa kuwa jumla ya watu 16,000 upoteza maisha kutokana na ajali hizo kila mwaka.

Poswayo alisema kuwa kutokana na taasisi yao kujishughulisha na masuala ya usalama wa barabarani katika bara la Afrika, waliamua kuzindua mpango huo hapa nchini kwa lengo la kuwalinda wanafunzi na watu wengine wanaotumia barabara wakati wa shughuli zao za kila siku.

Alifafanua kuwa mpango huo utahusisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ambayo itatumiwa na watembea kwa miguu, waendesha pikipiki, baiskeli na magari kuepuka ajali hizo ambazo nyingi zimeleta madhara kwa watu na wenginekubakia na ulemavu kama si kupoteza maisha. 
 Mkurugenzi wwa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo akikata utepe kuzindua mpango wa kuwalinda wanafunzi wa shule za msingi kupatwa na ajali za Barabarani ulionzishwa na Shirika la Amend kwa msaada wa taasisi ya Puma Energy na Taasisi ya Fia kwenye shule ya msingi Mpakani ya Manzese Tip Top. Wengine katika picha ni Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (wa tano kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Amend, Ayikai Poswayo (wa kwanza kulia) na Diwani Kassim Lema ( wa kwanza kushoto).
 Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo akizungumza katika uzinduzi wa programu ya kuboresha miundombinu ya usalama wa Barabarani kwa shule za msingi iliyoanzishwa na  Shirika la Amend kwa kushirikiana naTaasisi za Puma Energy na Fia. Mpango huo uliozinduliwa katika shule ya msingi Mpakani, Manzese Tip Top  umeanzishwa kwa lengo la kuwakinga wanafunzi wa shule za msingi kupata ajali za barabarani.  
 Mkurugenzi wa Mpango hu wa Shirika la Amend, Ayikai Poswayo kutoka Ghana akizungumza katika hafla hiyo.
 Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi, Thabitha  Makaranga akizungumza katika hafla hiyo. Makaranga aliwamwakilisha Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpiga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...