Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo Sido Mkoani Pwani Agnes Yesaya wa kushoto akiwa na Mwenyekiti wa kikundi cha Tuwenao wa kulia Sophia Mwaya mara baada ya kumkabishi cheki ya kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajii ya kikundi.

NA VICTOR  MASANGU , MKURANGA

SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani katika kuunga kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na wimbi la umasikini limevisaidia kuvikopesha vikundi viwili  vya ujasiriamali  kiasi cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya kuweza kuwasaidia kuendeshea katika shughuli zao za kilimo kwa kuweza kuzalisha na kusindika wenyewe zao la muhogo .

Akizungumza na baadhi ya viongozi na wajumbe wa vikundi  hivyo vya ujasiriamali vya Tuwenao pamoja  Mponga   vilivyopo Wilayani Mkuranga  katika halfa fupi ya kukabidhi cheki ya fedha iliyofanyika katika kiwanda kidogo cha kusindikia muhogo Meneja wa SIDO Mkoa wa Pwani  Agness Yesaya amesema kuwa wameamuakuvisaidia vikundi  vya wajasiliamari wadogo waliopo vijijini kwa lengo la kuweza  kuwawezesha ili kuwainua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Baadhi ya viongozi wa Sido wakiwa wanatoka katika kiwanda kidogo cha kusindika zao la muhogo kilichopo katika kijiji cha Mpongo Wilayani Mkuranga.

 Meneja Yesaya  alisema kwamba wamebaini katika maeneo mengi ya vijiji kuna fursa nyingi zilizopo katika zao la muhogo lakini wamebaini kuwepo kwa baadhi ya wajasiriamali wanshindwa kutimiza malengo yao waliyojiwekea kutokana na kukosa mtaji wa fedha hivyo wakiwezeshwa wataweza kutumia fursa zilizopo za kilomo kwenye   maeneo yao ili kuleta mabadiliko chanya ya kukuza uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...