Tunawashukurukwa kupokea wito wetu na kuja, karibuni sana tunawaahidi kwamba tutaendelea kushirikiana nanyi katika kila hatua.

Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unavipongeza sana vyombo vyote vya habari nchini kwa juhudi zenu za kuhabarisha, kuelimisha, kuwaasa, kuwaelekeza na kuihabarisha jamiii katika masuala kadhaa yanayohusiana na mipango ya maendeleo, mikakati, sera na malengo ya Serikali na mipango ya vyama vya siasa.

Ndugu Waandishi wa habari.

Tumewaita leo kuzungumzia mambo 2 makubwa, na suala zima la mtikisiko wa demokrasia katika mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulivyoendeshwa ndani ya vyama vya upinzani nchini.

Bunge la Afrika Mashariki kama mjuavyo ni chombo kikubwa na chenye heshima ya pekee katika kanda yetu. Kuwepo kwake kunaashiria muendelezo wa kufufua dhana, dhamira, mikakati, fikra na malengo ambayo yaliasisiwa na waasisi wa Mataifa yote yaliyomo katika Kanda yetu ili hatimaye siku moja ishuhudiwe Kanda hii na Bara zima la Afrika likiunda dola moja.

Ni jambo la heri na faraja kuona EAC ya sasa ikiwa ni yenye kufikia
malengo ya utengamano na mafanikio hususan katika nyanja za kiuchumi na kiusalama kama vile kuwa na Pasi moja ya kusafria, miingiliano ya
wananchi wake katika ufanyaji wa biashara pia mkakati kuelekea kupata
viwango sawia vya ushuru wa Forodha.

Masuala mengine ni kuona maeneo ya mipaka yetu kukiendelea kuwa na ustawi wa hali ya utulivu na usalama, wakati huo EAC ikifanya kila linalowezekana kumaliza migogoro yake ya kisiasa ambapo mazungumzo ya upatanishi huko Burundi yamekuwa yakiendelea chini ya mpatanishi mkuu Rais mstaafu Benjamin Mkapa sambamba na wananchi wa pande zote za nchi wanachama tukishuhudia wakiishi kwa maelewano, umoja, udugu na mafahamiano.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM,Shaka Hamdu Shaka .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...