Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ushirikiana na madaktari wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa wakati akielezea jinsi kambi hiyo ya upasuaji inavyoendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa.

Dkt. Nyangasa alisema, “Kwa kushirikiana na washirika wetu wa OHI tulianza kambi maalum ya upasuaji kuanzia tarehe 10/03/2017 hadi leo  tarehe 17/3/2017 tumefanya  upasuaji kwa wagonjwa 11 ambao wanaendelea vizuri,  kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima ni wawili”,.  

Dkt. Nyangasa alisema  katika kambi hiyo  ambayo inamalizika tarehe 17/3/2017 walipanga kufanya upasuaji kwa wagonjwa 25 kati ya hao watoto ni 15 na watu wazima ni 10.

Kuhusu uhitaji  wa damu kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa Moyo Dkt. Nyangasa alisema wagonjwa hao wanahitaji damu nyingi hivyo basi aliwaomba wananchi wajitokeze kuchangia  damu ambayo itatumika kwa wagonjwa.

“Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu na  uchangiaji huu wa damu  usifanyike mara moja bali  uwe endelevu  kwani Taasisi inatoa huduma kwa wagonjwa wakati wote siyo wakati wa kambi maalum za matibabu ya moyo pekee yake”, alisisitiza Dkt. Nyangasa.

Tangu kuanza kwa mwaka huu  wa 2017 JKCI kwa kushirikiana na baadhi ya washirika wake wa nje ya nchi ambao ni  Madaktari  Afrika wa  Marekani, Hospitali za  Apolo Bangalore na BLK zote za nchini  India na Open Heart International ya Australia wamefanya  matibabu ya moyo ya kufungua na bila kufungua kifua kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuziba matundu ya moyo kwa mgonjwa wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Taasisi hiyo. Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuvuna mshipa wa damu mguuni kwa mgonjwa wa moyo na kuupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba kwa jina la kitaalamu Coronary Artery Bypass Graft (CABG). Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili. Habari/Picha na Anna Nkinda – JKCI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...