THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANESCO YAKANUSHA TAARIFA YA DAWASCO
TAARIFA:


SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) linakanusha Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maji Safi na Maji taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), kuhusu kukosekana kwa Huduma ya maji kwa siku ya Jumapili  tarehe 12/03/2017 kwa wakaazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani  ili kupisha TANESCO kufanya matengenezo ya ukamilishaji kazi ya  kuunganisha umeme kwenye mtambo mpya wa maji wa Ruvu Juu.

Aidha, Taarifa hiyo ya DAWASCO iliainisha kuwa ukosefu huo wa Huduma ya maji unatokana na matengenezo yatakayofanywa na TANESCO kwa siku husika.(12/03/2017).
TANESCO inapenda Umma ufahamu yafuatayo;
Mosi,  TANESCO ilipokea ombi  la DAWASA kupitia Mkandarasi wao (M/s Mollel Electrical Engineering) wiki iliyopita la kuomba kuzimwa umeme ili wakamilishe kazi ya mradi wa kuongeza mashine za kusukuma maji kwenye kituo cha Ruvu juu kilichopo Mlandizi, kupitia mradi huo mashine nne zinazohitaji megawati 2 kila moja zimefungwa.
Wataalam wa TANESCO waliishauri DAWASA wajenge laini ya kilovolti 33 kutoka Chalinze hadi Mlandizi ili kuzipatia umeme  mashine hizo mpya walizoongeza.
Pili,  Baada ya wataalam wa TANESCO kutembelea eneo hilo na kufahamu uharaka wa mradi huo wa maji kwa Wananchi ilishauri DAWASCO kwa barua kuwa umeme uzimwe siku ya ijumaa tarehe 10/03/2017 ili Mkandarasi wa DAWASCO kufanya kazi hiyo, ushauri ambao DAWASCO iliupinga wakiomba umeme uzimwe siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ili wapate muda wa kuwaarifu Wateja wao na TANESCO iliridhia.
TANESCO imeshangazwa na Taarifa hiyo ya DAWASCO kuwa TANESCO inafanya matengenezo ambayo yatapelekea ukosefu wa huduma ya maji huku ikitambua TANESCO inatekeleza ombi lao walilolileta.
Tunasisitiza kuwa,  taarifa za TANESCO kufanya matengenezo si za kweli na uzimaji umeme siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ni kwa ajili ya kupisha Mkandarasi wa DAWASCO kufanya kazi kama walivyoomba na  si TANESCO.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.