THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANTRADE yawapiga msasa watendaji kata 23 Temeke

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) , Bw. Edwin Rutageruka akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya biashara na ujasiriamali kwa maofisa watendaji kata wa manispaa ya Temeke kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(Tan Trade). Kushoto ni Mchumi wa Manispaa ya Temeke Bw. Erick Kilangwa. Na kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa TANTRADE, Bi.Anna Bulondo.
chumi wa Manispaa ya Temeke Bw. Erick Kilangwa (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya biashara na ujasiriamali kwa maofisa watendaji kata wa manispaa hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE,Bw.Edwin Rutageruka. Na kushoto ni Mchumi wa TANTRADE, Bw.Emmanuel Miselya. Mafunzo hayo yameratibiwa na TANTRADE.
Watendaji Kata wa Manispaa ya Temeke wakifatilia mada kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE) , Bw. Edwin Rutageruka katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ya biashara na ujasiriamali lenye lengo la kuwajengea uwezo kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa na TANTRADE.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE) , Bw. Edwin Rutageruka akifurahi jambo na Mchumi wa Manispaa ya Temeke Bw. Erick Kilangwa mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya biashara na ujasiriamali kwa maofisa watendaji kata 23 za manispaa hiyo kwa lengo la kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kutambua fursa za biashara zinazotolewa na TANTRDE.