TFF YAGONGA MWAMBA TRA, OFISI ZAENDELEA KUFUNGWA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeendelea kuwa katika sintofahamu baada ya ofisi zake kufungwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) baada ya kuwa na malimbikizo ya mda mrefu.

Maofisa hao kutoka kampuni ya YONO Auction Mart walipewa mamlaka na TRA ya kufungia ofisi hizo za TFF huku wakiwambia hawaruhusiwi kuendelea na kazi mpaka pale watakapomalizana na TRA.

Kwa mujibu wa deni hilo, TFF wanadaiwa deni la nyuma ambalo lilikuwa chini ya uongozi wa Leodigar Tenga ikiwemo kodi ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Marcio Maximo na kodi ya mechi ya Taifa Stars na Brazil.

Katika sakata hilo ambapo timu ya Serengeti Boys ipo kambini ndani ya Shirikisho hilo, wameendelea kusalia lakini wamepewa masharti ya kutokutumia uwanja huo kwa mazoezi mpaka pale watakapomalizana na TRA.

Baadhi ya viongozi wa TFF walijaribu kwenda ofisi za TRA mkoa wa Ilala kujua ni jinsi gani wanalimaliza sakata hilo liligonga mwamba na kushindwa namna ya kujikwamua kwenye adha hiyo.
 Maofisa wa Yono Auction wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TFF wakiwapa maelezo ya kutokuendelea kuwepo ndani ya viunga vya ofisi hizo
 Ofisi za TFF zikiwa zimefungwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...