THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TTB NA MAURTIUS KUUNGANISHA NGUVU KATIKA KUTANGAZA UTALII.

Na: Geofrey Tengeneza -Berlin

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano baina yao katika kutangaza wa nchi hizo mbili kwa pamoja katika baadhi ya masoko ya masoko ya Marekani, China, Australia, India na masoko mengine barani la Ulaya. 

Mkataba huo uliosainiwa leo katika maonesho ya Utalii ya ITB na wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo ambao ni Bi Devota Mdachi kwa upande wa Bodi ya Utalii Tanzania na Bw. Kelvin Ramkaloan kwa upande wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius una lengo kuvutia watalii zaidi kutoka barani Ulaya, Amerika na Asia. 

Akizungumzia mkataba huo Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi amesema kuwa katika mkataba huo wamekubaliana kushirikiana katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi hizo mbili sambasamba na kuhakikisha kuwa watalii wanaotembelea Mauritius ambayo ni maarufu kwa utalii wa fukwe wanatembela pia Tanzania kwa ajili ya utalii wa kutazama wa wanyama katika hifadhi zetu mbalimbail za Taifa , kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea maeneo mengine ya vivutio vya utalii. 

“Tutazitangaza nchi zetu kama maeneo pacha ya utalii lengo likiwa ni kutumia fursa ya watalii wanaotembelea Mauritus kwa ajili utalii wa fukwe kuunganisha safari zao na kujakutembela pia Tanzania kupitia shiika la ndege la Mauritus kwa ajili ya kujionea vivtio vyetu kama vile wanyama , mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na vingine vingi ambavyo Mauritus hawana.” alisema Bi Devota Mdachi.

Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo akibadilishana mawazo na Mkuu wa Idara ya mauzo ya shirika la ndege la Condor Bw. Andre Horn muda mfupi baada ya TTB na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius kusaini makubaliano ya ushirikiano.