Na Geofrey Tengeneza - Berlin

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeingia mkataba na kampuni tatu za Ulaya na Marekani ili kutayarisha mikakati maalumu ya utangazaji utalii mahsusi katika nchi za Ujerumani, Uingereza na Marekani ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha inajipenyeza zaidi kaika masoko ya makuu ya utalii yalioanishwa katika mkakati wa Utangazaji utalii wa kimataifa wa miaka mitano katika masoko mbalimbali ya utalii duniani.

Mkataba huo umesainiwa katika maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB katika banda la Tanzania na Mkurugeni Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi na Wakurugenzi wakuu wa kampuni hizo ambazo ni Africa Oracle Company kwa ajili ya soko la Uingereza, 7o7 Marketing GmbH Ltd kwa ajili ya soko la Ujerumani na Tourism Intelligence International kwa jili ya soko la Marekani.
Bw. Recknagel Markus, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya7o7 Marketing GmbH ya ujerumani na Mkurugenzi mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi wakionyesha jarida la TTB lililotayarishwa kwa lugha ya Kijerumani kwa lengo la kuutangaza utalii na vivutio vya utalii vya Tanzania katka soko la ujerumani na nchi zinazozungumza Kijerumani.

Kwa Mujibu wa Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena pamoja na kuwa mkakati wa Kimataifa wa miaka mitano umeainisha masoko kumi na mbili ya utalii duniani, wameamua kuanza na masoko hayo matatu kwa kuwa ni miongoni mwa masoko muhimu kwa Tanzania hivi sasa. Masoko makubwa manne yanaoongoza kwa watalii wengi kutembelea Tanzania ni Marekani, Uingereza, Italia na Ujerumani.

“Kwa kuanzia tumeanza na masoko haya na baadae tutakwenda pia katika masoko mengine. Wataalamu hawa kutoka masoko hayo matatu wakikamilisha kututayarishia mikakati hiyo maalumu kwa kila soko itatusaidia kujua mbinu gani sahihi za kujipenyeza na kulikamata kikamilifu kila soko” alisema Bw. Meena

Kusainiwa kwa mikataba hii kumefanyika siku moja tu baada ya Bodi ya Utalii Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius katika utangazaji wa pamoja wa utalii wa nchi hizo mbili.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi Devota Mdachi (kushoto) na Dr. Auliana Poon Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni Tourism Intelligence International wakisaini mkataba kwa ajili ya mkakati wa TTB kwa ssoko laMarekani huku Mwenyekiti wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akishuhudia utiaji saini huo.
Bi Devota Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji w TTB akibadilishana mkataba na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya 7o7 Marketing GmbH Limited Bw. Recknagel Markus mara tu baada ya kusaini mkataba huo kwa ajili ya soko la Ujerumani.
Dr. Auliana Poon wa Kampuni ya Tourism Intelligence International ya Marekani akibadilishana mkataba na Bi Deota Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB mara baada ya kusaini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...