Tanzania, Sio Salama kabisa Kimtandao na kumekua na matukio kadhaa ya kujaribu kushambulia TRA pamoja na mashirika mengine.
Tanzania, Ambapo imeendelea kuonekana ikikusanya pesa nyingi - Imekua ikiangaziwa macho na wahalifu Mtandao.
Binafsi, Nimesha chukua hatua kadhaa ya kukutana na TRA kuhusiana na matishio ya kimtandao - Na walikiri kupokea mashambulizi mengi huku wakisema wamechukua hatua za kuwasilisha malalamiko eGA.
Niliwashauri washirikishe vitengo vingine kama TZ-CERT na CYBERCRIME UNIT paamoja na wadau wengine ili kuhakiki wanakomesha majaribio hayo ya kihalifu kimtandao ambayo yanaweza kuligharimu Taifa na kusababisha Hasara kubwa.
Itakumbukwa hivi karibuni, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Alizungumzia swala la uhalifu mtandao katika Shirika la Ndenge Tanzania.
Naendelea kutoa wito, Tufunge mikanda ili tuweze kuwabaini wahalifu Mtandao pamoja na kuwachukulia hatua stahiki
Kenya, wameonyesha nia ya kukabiliana na hali hii kwa dhati na Tanzania tuongeze nguvu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...