Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kuelekea kwenye mtanange wa Ligi Kuu Vodacom kati ya Yanga na Azam, Nahodha msaidizi wa timu ya Yanga kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima ameongelea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa. 

Niyonzima amesema kuwa  wao kama wachezaji wamejiandaa vyema kisaikolojia kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Azam  ili kuzipata alama tatu muhimu katika harakati za kulitetea kombe lao wanalolishikilia .

" namshukuru mungu  binafsi nipo vyema kwa ajili ya mchezo wa kesho, mwalimu akinipa nafasi hakika nitatimiza majukumu yangu vyema pamoja na wenzangu ili kuhakikisha timu yetu inashinda ,"amesema Niyonzima 

Amesema kuwa waalimu wanawaandaa vyema kushinda mchezo huo na mingine iliyobaki ili kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu . 

Niyonzima alienda mbali zaidi kwa kuwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti ili kuwatia nguvu kwa dakika zote 90. 

" naheshimu sana mchango wa mashabiki wetu katika timu hii  na kulitambua hilo  nawaomba kesho wajitokeze kwa wingi ili kutupa sapoti , ari na nguvu ya kupambana muda wote wa dakika 90 dhidi ya Azam FC kwani ni timu nzuri na sote tunajuana vyema hivyo umakini unahitajika katika kuwakabili, "amesema Niyonzima.

Yanga itawakosa mabeki wake wawili Hassan Kessy na Kelvin Yondani kwa kuwa na kadi  tatu za njano ila mpaka sasa uhakika wa washambuliaji wake wawili Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi Amisi Tambwe ambao bado  ni majeruhi wa goti.

Yanga kesho tarehe 1 , April watakuwa uwanja wa taifa kupepetana na Azam FC katika mchezo wa 25 wa ligi kuu Tanzania bara kuelekea ukingoni mwa ligi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...