Na. Immaculate Makilika –MAELEZO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim wanatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu (Ubungo interchange) eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam Machi 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inasema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo yatagharimu takribani shilingi bilioni 188.71 ambapo una lengo kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma.

“Mradi huo ni sehemu ya uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania”

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa, mradi huo utahusisha pia awamu ya tatu na ya nne ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit- BRT), katika barabara ya Nyerere kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la mboto na barabara ya Bagamoyo kutoka katikati ya jiji hadi Tegeta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...