NA ESTOM SANGA-TASAF.

Wahenga walinena ‘’mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe’’na ‘’penye nia pana njia’’ni semi zilizoanza kuonekana kwa vitendo miongoni mwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Baadhi ya walengwa wa Mpango huo wameanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika mafuta ya mawese kwa kutumia fedha za ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia TASAF.

‘’ Baada ya kupata fedha za TASAF niliamua kununua mbegu za mawese na kisha kuanza kuzisindika kwa lengo la kukamua mafuta ya mawese na hadi sasa nimepiga hatua ya kujivunia’’ ninaishukuru sana serikali na TASAF amesema bi.Coletha Emilliani Nipala mkazi wa eneo la Mbasa katika mji wa Ifakara.

Anasema mbali ya changamoto ya udogo wa mtaji hajakumbana na tatizo la soko kwani mafuta ya mawese yanahitajika kwa kiwango kikubwa kwa matumizi ya walaji na hata kutengenezea sabuni.

Bi.Lucia Ngalota (aliyevaa kitambaa kichwani) mkazi wa kijiji cha chita wilaya ya Kilombero akiwaonyesha waandishi makazi yake mpya aliyoijenga baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF.
Hii ni nyumba aliyokuwa akiishi bi Lucia kabla ya kuorodheshwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ambayo imeanza kubomoka.
Nyumba ya walimu iliyojengwa TASAF kupunguza tatizo la makazi kwa walimu katika shule ya msingi Mbasa shule anbayo pia kuna wanafunzi kutoka kaya za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini.
Mbali na kutoa ruzuku kwa walengwa, TASAF pia imeendelea kujenga majengo ya shule na nyumba za walimu kama anathibitisha Mkuu wa Shule ya msingi Mbasa katika wilaya ya Kilombero Mwl. Aman Ngowi akihojiwa na waandishi wa habari juu ya ujenzi wa nyumba inayoonekana nyumba yake.
Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Mbasa wilaya ya Kilombero Bi. Coletha Emilian Nipala (aliyevaa kitambaa chekundu kichwani) akihojiwa na Waandishi wa Habari namna alivyoweza kutumia fedha zaruzuku kutoka TASAF kuanzisha kiwanda kidogo cha kusindika mawese na kujiongezea kipato.Picha ya chini ni mbuzi anaowafuga baada ya kununua kwa ruzuku kutoka TASAF.
Bi. Victoria Johnson Nguge mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Chita akihojiwa na Waandishi wa Habari juu ya mafanikio aliyoyapata tangu aorodheshwe kwenye Mpango ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...