THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WANANCHI MKURANGA WAPATA HUDUMA ZA VIPIMO VYA AFYA ZAO BURE

 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Wananchi wa Mkuranga wametakiwa kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali na pale wanapokutwa kuweza kutibu kwa wakati mwafaka.

Akizungumza katika upimaji wa Afya huo,Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo amesema kuwa katika dunia ya sasa jamii inawajibu wa kupima afya kujua ana tatizo au hana ili kuweza kuchukua hatua pamoja na kujinga na magonjwa mbalimbali yanatokana na mfumo wa maisha.

Othman amesema kuwa huduma hiyo itatolewa  kwa wa wananchi wa Mkuranga, Vikindu, Mwanambaya, Mbagala na maeneo  mengine yaliyo karibu.

Amesema wamechagua Wilaya hiyo kutokana watu wengi wanashindwa kuifikia na kuona kwa taasisi hiyo inawajibu wa kupima afya za wananchi ha.

Aidha amesema kuwa watu wengine ambao wanauwezo wajitokeze katika kutoa huduma ya upimaji ili waweze kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na mfumo wa maisha.

Amesema tangu jana walipoanza kupima watu zaidi ya 500 wamwjitokeza kupima na mwitikio umekuwa  mkubwa wa kuweza kuvuka malengo ya upimaji huo.

Huduma ya vipimo walivyotoa ni Msukumo wa Damu (BP), Sukari , Unene na Urefu kuendana sawa na mwili (BMI) Ushauri Nasaha  na Upimaji wa VVU,Utafiti wa Saratani ya matiti pamoja na utafiti wa Saratani ya Kizazi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan Tanzania, Othman Kaporo akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa upimaji wa afya kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga leo.
  Muuguzi Mariam Adamu akipima kipimo cha Sukari na Msukumo wa Damu
 Wananchi wakisubiri huduma ya vipimo vinavyotolewa na Taasisi ya Ibun Jazar leo.