Wanawake na vijana ni nyenzo muhimu katika uhamasishaji wa kumaliza machafuko yanayoendelea nchini Somalia, wakati kundi hilo pia likilengwa zaidi na vikundi vya kigaidi kutumika katika matukio ya kigaidi. 

Hayo yamebainishwa na Bi. Mane Ahmed, Afisa Jinsia kutoka African Union Mission in Somalia (AMISOM), wakati wa mkutano wa siku tatu unaomalizika leo (Ijumaa) jijini Dar es Salaam jana.

Mkutano huo ulioandaliwa na AMISOM kwa ushirikiano na serikali ya Somalia unalenga kutafuta njia stahiki za kuzuia vijana kudahiliwa na vikundi vya kigaidi nchini humo.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umebainisha umuhimu wa ujengaji uwezo kama hatua madhubuti katika kueneza hali ya kuvumiliana ndani ya jamii na kuwapa sifa mbaya Al-Shabaab.

Akizungumza mkutanoni hapo, Bi Mane amesema kuwa Serikali ya Somalia imeanzisha ofisi ijulikanayo kama Counter-Violent Extremism (CVE) ikiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kukamilisha rasimu ya kwanza ya Sera ya Kuzuia na Kupambana na Vikundi vyenye msimamo mkali.

Bi Mane alisema kuwa AMISOM imeanzisha Mtandao wa Kijinsia ambao umelenga katika kuzuia na kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali kwa lengo la kusaidia juhudi za Shirikisho katika kuunganisha mtazamo wa kijinsia katika mpango na mikakati yake.

Bi Muna alisema: "Mkutano huu utawajengea uwezo viongozi wa dini, watendaji wa Somalia na kuongeza ufahamu wao juu ya umuhimu wa kuwajumuisha wanawake katika njia yao za kupambana na siasa kali na kubadilishana uzoefu na mbinu bora na wataalamu, watafiti, watendaji kutoka barani ambao wana ufanisi mkubwa katika kukabiliana na masuala yahusuyo vikundi vyenye misimamo mikali."

Bi. Mane Ahmed, Afisa Jinsia kutoka African Union Mission in Somalia (AMISOM) akizungumza na waandishi wakati wa mkutano huo.

Washiriki wa mkutano huo wakifatilia mada zilizowasilishwa wakati wa mkutano huo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...