Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania Gerson Lwenge ameishukuru Kuwait kwa kusaidia miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa hapa nchi na kueleza kuna anatarajia ushirikiano zaidi hasa katika miradi ya umwagiliaji.
Kupitia mikopo mbalimbali inayotolewa na Mfuko Wa Kuwait Wa Maendeleo ya Kiuchumi kwa miradi mikubwa ya umwagiliaji.
Waziri Lwenge alitolea mfano wa mradi wa hivi karibuni katika mikoa ya Same na Mwanga, Kaskazini mwa Tanzania, mradi ambao una thamani ya dola za marekani milioni 34.
Waziri pia aligusia miradi mingine miwili ya umwagiliaji katika bonde la Muhongo na Luichi kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambayo ina thamani ya dola za marekani milioni 15.
Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait unatarajia kutuma wataalamu wake Tanzania kwa lengo la kutathmini miradi hii miwili katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018.
Waziri pia alitoa Pongezi na shukrani zake za dhati kwa ujumbe wa Kuwait Red Crescent Society uliofanya ziara nchini Tanzania hivi karibuni na kufungua visima 16 katika shule mbalimbali za serikali ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Kisima kwa Kila Shule.
Ikumbukwe kuwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassim Al Najema ameanzisha mpango huo wa Kisima kwa Kila Shule kuunga mkono wito wa Rais John Magufuli wa kusaidia sekta ya elimu nchini na kukabiliana na ukame na uhaba wa maji safi ya kunywa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...