Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kagera kwa hatua iliyofikiwa
katika kurejesha miundombinu mbalimbali iliyoathiriwa na tetemeko la
ardhi lililotokea Septemba10 mwaka 2016 katika Mkoa wa Kagera
linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya Richter.
Mhe. Mhagama alionesha kuridhishwa
kwake baada ya kufanya ziara Mkoani hapo mapema wiki hii kwa lengo la
kutathimini utekelezaji unaoendelea katika kurejesha miundombinu ili
wananchi waendelee kutumia huduma hizo kama kawaida.
Katika ziara hiyo, Waziri
Mhagama alitembelea Shule ya Sekondari Nyakato, Ihumo na Omumwani, Kituo
cha Afya cha Kabyaile-Ishozi na Kituo cha Kulelea Wazee cha Kiilima na
kubaini kuwa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Kabyaile-Ishozi ambacho
kimefikia asilimi 80 ambapo kimetumia kiasi cha shilingi 381, 506,
079.00.
“Nikiri kwamba ukiacha baadhi
ya mapungufu kwa watendaji wachache, wengi mmetupa ushirikiano mzuri kwa
kulinganisha hali ilivyokuwa kwa kuangalia tukio lilivyotokea na hadi
hatua za kukabili hatimaye kurejesha hali.”Alisema Waziri
Aliendelea kushukuru
ushirikiano mzuri uliopo katika kutekeleza majukumu hatimaye kufikia
lengo “Kama sio ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu,
Ofisi ya Mkoa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania huwenda tusingefika hapa
hivyo tuna kila sababu ya kupongeza juhudi hizi kwa niaba ya Serikali
hususani Ofisi ya Waziri Mkuu tumefarijika kwa ushirikiano wenu”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akinukuu hoja za wajumbe wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili na Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko Mkoani Kagera kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkoa Machi 18, 2017 kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili na Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kujadili na kupokea taarifa hiyo mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo akichangia hoja wakati wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji ya Kukabili na Kurejesha hali baada ya athari za tetemeko mkoani Kagera.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...