THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA WFP, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

FUKU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya WFP na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. 
FUKU 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford, wakati kiongozi huyo alipomtembelea Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Shirika lake na Tanzania. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.
FUKU 2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford, wakati kiongozi huyo alipomtembelea Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya WFP na Tanzania. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.