Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano itayoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas kuchunguza tukio la uvamizi lilofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika chombo cha habari cha Clouds Media.
Akiongea katika ziara aliyoifanya  leo  Jijini Dar es Salaam  katika chombo hicho Mhe.Nape amesema Kamati hiyo itafanya kazi ndani ya masaa 24 kuanzia sasa huku akiwataja wajumbe wengine  kuwa ni Bw. Frank Balile,Bibi.Johanes Neng’ida,Bw.Jessy Kwayu na Bibi. Mabel Mabisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Serikalini (TCRA).
“Kamati hii ipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Paul Makonda ili tuwe na taarifa iliyokamilika na kujua hatua itakayofuata” alisema Mhe.Nape
Aidha Waziri Nape ameeleza kuwa kitendo cha uvamizi kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa kipo kinyume na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kwa kuwa sheria hiyo ipo kwa ajili ya kulinda wanatasnia hao.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika Picha) alipofanya ziara katika Chombo cha Habari cha Clouds leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Katikati, akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) Bw. Reginald Mengi (kulia) alipofanya ziara katika chombo cha Habari leo Jijini Dar es Salaam ,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbas.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Bw.Joseph Kusaga (wa pili kushoto) alipowasili katika ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam, wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas (pembeni ya Waziri) na wa kwanza kushoto ni Afisa Mahusiano wa Clouds Bw. Simon Simalenga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...