Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye (pichani juu kabisa) amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano ya Rais, Ikulu, 
 na Idara ya Habari MAELEZO kwa ubunifu na weledi wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano.
Waziri Nape alisema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili Maafisa Mawasiliano wa Serikali wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali ,amewataka kuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano hasa mitandao ya kijamii katika kutekeleza majukumu yao kwani ni nafuu na rahisi.  
“Nawapongeza sana wakurugenzi vijana Dkt. Hassan Abbasi wa MAELEZO na Greyson Msigwa wa Ikulu. Hawa ni mfano wa ubunifu  wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa”alisema Waziri Nape.
Waziri Nape aliongeza kuwa pamoja na ubunifu wao katika mitandao ya kijamii, utayarishaji wa makala za Serikali na kujibu hoja kwa haraka kupitia taarifa kwa umma,  wameweza pia kubuni vipindi vya TUNATEKELEZA na SAFARI YA DODOMA ikiwa ni mkakati wa kusukuma mbele ajenda za Serikali.
Aidha, Waziri Nape amewataka Maafisa Mawasiliano kutumia fursa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari binafsi  kupitia vipindi vya bure kwenye Televisheni, redio na magazeti  kuhakikisha mambo mazuri yanayotekelezwa na Serikali yanatangazwa na kuweza kusikika kwa Wananchi.
“Nimezungumzia hoja na haja ya mabadiliko kiutendaji, lakini nikiwa kiongozi ambaye pia katika maisha yangu nimefanya kazi ya kuongoza kitengo cha habari na uenezi nafahamu changamoto zinazoikabili kada hii,lakini unaweza ukageuza changamoto kuwa fursa,kwahiyo tujiongeze ndugu zangu ” alisema Waziri Nape. 
 Waziri Nape alitoa wito kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi,Wakuu wa Taasisi pamoja na watendaji wakuu katika ofisi za umma kuhakikisha wanatenga fedha katika bajeti kwaajili ya kununua vifaa vya kutendea kazi ili kuviwezesha vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi katika kuisemea Serikali.
6

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...