Habari Picha na Imma Msumba.

Waziri wa Elimu na Sayansi Prof. Joyce Ndalichako mapema leo asubuhi amewasili katika Chuo cha Sayansi na Tekinolojia Nelson Mandela Arusha kwa ajili ya Uzinduzi wa mpango wa African Capacity unaofadhiliwa na Benki ya ADB.
 
Akizungumza na wanafunzi wa Chuoni hapo Profesa Ndalichako amesema Atawachukulia hatua kali waajiri katika sekta ya Elimu watakaowakataza baadhi  ya wafanyakazi waliopata ufadhili wa kwenda masomoni kujiendeleza .

Pia akiwa kwenye uzinduzi huo waziri alifanikiwa kutembelea maabara mbalimbali za idara tofauti za Chuo hicho zinazotumika na wanafunzi kwa ajili ya majaribio na pia alipata wasaaa wakutembelea shamba la migomba lililopo nje kidogo ya chuo hicho.
Waziri wa Elimu akisalimia na watumishi ya Chuo cha Nelson Mandela leo Asubuhi baada ya kuwasili chuoni hapao . Waziri wa Elimu profesa Joyce Ndalichako ( katikati ) Akimsikiliza Mkuu wa Maabara ya Taasisi ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandela jijini Arusha .
Pichani ni wanafunzi wa PHD in material science and Energy lub,Agatha Wagotu na Joyce Elisadiki wakiwa ndani ya Maabara wakifanya majaribio.
 
 
  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...