THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI SIMBACHAWENE:MAAFISA UTUMISHI KUWENI WAADILIFU

Na. Vero Ignatus, Arusha.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaagiza maafisa utumishi kuwa waadilifu na wakweli katika kutunza nyaraka zinazowahusu watumishi wenzao.

Aidha serikali inatambua kuwa inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii na inajitahidi kulipa madeni hayo inayodaiwa na mifuko ya Hifadhi za Jamii .

Simbachawene amesema hayo wakati akifungua mkutano wa tisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema baadhi ya maafisa utumishi wamekuwa kama miungu watu na kupoteza nyaraka za watumishi huku wanapobanwa na waajiriwa kuhusu taarifa za watumishi husema uongo  wakijua wenzao wanafamilia kama wao.

Pia amekemea tabia ya watumishi wa masijala ambao wanapoteza kumbukumbu za watumishi kwa makusudi hali inayosababisha baadhi yao kupunjwa madai yao kutokana na baadhi ya kumbukumbu kupotezwa.

"Nawaomba nyie maafisa utumishi muwe makini sana na maisha ya watumishi wenzenu oneni huruma kwao mnapoteza kumbukumbu au kutoa ruhusa kwa watumishi halafu mkibanwa mnasema hamna taarifa hii inawaumiza watumishi wenzenu maana wanafamilia zao kwanini muwafanyie mambo yasiyofaa mjirekebishe nyie pamoja na watu wa masijala ".

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Lapf, Profesa Faustine  amesema kuwa mfuko huo unajitahidi kutoa huduma kwa wakati ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama na kubuni mbinu za kukuza uchumi katika sekta ya viwanda.

Alisema mfuko huo utaendelea kutoa huduma kwa wakati akiwemo fao la kulipwa jana kwa wanachama wastaafu sanjari na kutoa mkopo wa maisha popote unaotolewa kwa waajiriwa wapya kwakushirikiana na Benki ya CRDB.

Naye Mkurugenzi wa mfuko huo, Eliud Sanga alishukuru wanachama hao kwa kushiriki katika mkutano huo sanjari na kuuchagua mfuko huo ambao utatoa jana na hivi sasa wapo katika uchambuzi wa Kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Tanga, Kiwanda cha Kuchataka nyama kilichopo Morogoro pamoja na kiwanda cha vifaa vya hospitali Mkoani Shinyanga ambapo miradi hiyo itaanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka huu.

 Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tamisemi mhe,George Boniface Simbachawene